
- 2019/06/06
- 08:00 AM
Katika kuadhimisha siku ya bahari duniani ” World Ocean Day”, ambayo huadhimishwa tarehe 08 June ya kila mwaka, Kampuni ya Coca Cola Kwanza Tanzania kushirikiana na wadau mbalimbali tukiwemo Sukos Kova Foundation, Red Cross, vikundi vya jogging, vikoba n.k tulishiriki kwa pamoja katika kufanya usafi Kibo beach ikiambatana na Elimu ya utoaji wa huduma ya kwanza iwapo mtu anapata ajali au majeraha katika eneo la bahari au ufukweni iliyotolewa na Sukos Kova Foundation kushirikiana na Red Cross Tanzania, mazoezi na michezo mbalimbali. Yote hii ikiwa ni katika muendelezo wa kampeni ya Coca Cola Kwanza Tanzania iitwayo “Mchanga Pekee” yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira.



