
- 2019/03/08
- 08:00 AM
Taasisi ya Sukos Kova Foundation tumeungana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama siku ya leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 08/03/2019 kupitia kuhamasisha wanawake kujitolea damu zaidi.
Lengo likiwa ni kuongeza ushiriki wa wanawake katika zoezi la kujitolea damu ili kuokoa Maisha ya Mama na mtoto kwani takwimu zinaonyesha asilimia 14% ya wanawake ndio hushiriki kujitolea damu kulingana na wanaume ilhali wahanga na wahitaji wakubwa wa damu huwa ni wanawake.



