logo

May 13 2025

SUKOS KOVA YAKABIDHI VIFAA MAAFA YA KARIAKOO

Taasisi ya Sukos Kova Foundation kwa kushirikiana na Peaceland Foundation imetoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na Janga lililotokea katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sukos Kova Foundation; Kamishna Mstaafu Suleiman Kova amekabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila huku akiwasilisha salam za pole kwa majeruhi wote na familia zao pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao kutokana na Janga hili.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na;
1. Hard Gloves = 20 pieces
2. ⁠Safety Helmets = 70 pieces
3. ⁠Rescue Torch = 10 pieces
4. ⁠Normal Torch = 20 pieces
5. ⁠Face Masks = 15 boxes
6. ⁠Examination Gloves = 22 boxes
7. ⁠Pain Killers = 27 boxes
8. ⁠Reflectors = 20 pieces
9. ⁠Water Cartons = 120 Cartons
10. ⁠Tents = 2 Tents

Aidha Kamishna Mstaafu Kova ameahidi kuwa Taasisi ya Sukos Kova Foundation kwa kushirikiana na Peaceland Foundation wapo tayari kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na Majanga nchini

admin

Leave A Comment

Our Maps

© Copyright of sukosdmkovafoundation