logo

May 13 2025

SUKOS YAIKABIDHI BOTI SERIKALI KWA AJILI YA UOKOAJI 

TAASISI YA SUKOS KOVA FOUNDATION YAIKABIDHI SERIKALI BOTI MAALUM YA UOKOAJI PAMOJA NA KUTOA MAFUNZO YA UOKOAJI KWA VIKOSI VYA UOKOAJI PAMOJA NA JAMII.

Taasisi ya Sukos Kova Foundation kwa kushirikiana na Peaceland Foundation imeikabidhi Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Boti ya Uokoaji katika Maji (Marine Rescue Boat) pamoja na vifaa mbalimbali vya uokoaji katika maji ikiwemo Jaketi okozi “Life Jackets” kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na Maafa na Majanga nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Sukos Kova Foundation Kamishna Mstaafu Suleiman Kova amesema Taasisi ya Sukos Kova Foundation inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Serikali yetu chini Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan hasa katika juhudi za kukabiliana na Maafa na Majanga nchini. Hivyo, kwa kulitambua hilo, Sukos Kova Foundation imepokea boti tatu kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya Uokoaji kwa vikosi mbalimbali vya Uokoaji ambapo Boti moja imekabidhiwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na mbili zitatumika na Taasisi ya Sukos kuendesha mafunzo endelevu ya Uokoaji kwa vikosi na vikundi husika. Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu wetu waweze kutambua mbinu mbalimbali za Uokoaji ili pindi majanga yanapotokea waweze kusaidia kuokoa watu na mali hivyo kusaidia kupunguza athari zitokanazo na Majanga/ Maafa nchini Tanzania.

Tags:

admin

Leave A Comment

Our Maps

© Copyright of sukosdmkovafoundation